FASHION ZA VIATU VYA WANAWAKE


  Kuna fashion nyingi sana za viatu vya wanawake kwa sasa duniani. Fashion hizi za viatu Mara nyingi hutegemea sana mavazi, mitindo ya nywele na sehemu ambayo viatu vinavaliwa bila kusahau rangi ya mavazi ulovaa. mfano: darasani Kama ni mwalimu, ofisini, kwenye sherehe n.k

Ungana nami katika hii ya fashion za viatu vya kike. Hata tutajadili fashion moja na nyingine mpaka utakapopata uwezo wa kuchagua wapi na viatu vipi uvae. 

SIMPLE SHOES... (VIATU VYEPESI)

Viatu hivi huvaliwa na wanawake wa aina zote. Viatu hivi Mara nyingi havichagui mavazi Wala sehemu ya kuvivaa viatu hivyo...

Viatu hivi havina visigino virefu na wakati mwingine huvaliwa kwa kuingiza mguu wote na hufunika mpaka vidole. 

Wataalamu wanashauri uvaaji wa simple shoes kwa watu wenye pilika pilika au harakati nyingi zinazojumuisha kutembea. Viatu hivi hupunguza maumivu ya miguu na mchoko wa Mara kwa Mara... Wataalamu huenda mbali na kusema viatu hivi ( simple shoes) hupunguza matatizo ya miguu kwa wanawake wakati wa uzeeni.

Mwandishi: MEIMA

HONE: O757169470

Comments

Popular posts from this blog

FASHION YA SAA ZA MKONONI.