MAANA YA FASHION
fashio ni usemi wa urembo unaofahamika kwa wakati na mahali na kwa kazi maalum,haswa katika mavazi,viatu,mtindo wa maisha,vifaa, Mtindo mapambo,nywele na uwiano wa mwili.
Mitindo ni usemi tofauti na unaopewa kipaumbele na tasnia ambao kwa kawaida umefungamana na msimu wa mitindo.
Mtindo ni usemi unaodumu kwa misimu mingi na mara nying huunganishwa na mambo ya kitamaduni na alama za jamii,darasa kwa mfano Baroque,Rococo,n.k
Kulingana na mtaalaam wa sosholojia Pierre Bourdieu,mitindo inamaanisha …’’mitindo ya hivi karibuni,tofauti ya hivi karibuni’’ kutokana na utandawazi siku hizi mitindo inaentea duniani kote hasa kutoka nchi tajiri kwenda nchi maskini
Mitindo huwasilisha swala zima la urembo ambapo huleta muonekano mzuri zaidi hata hivyo mitindo huhitaji ubunifu zaidi ili kuwa na muonekano tofautitofauti katika mitindo. Hata hivyo haya yote hutegemeaa na misimu ya mwaka yaani masika,kiangazi,demani na kipupwe.
Kwa kuanza kuzungumzia suala zima la mitindo ya vito kama vile hereni,saa,bangil,vikuku,shanga ,mapambo dhahabu ya nywele n.k…ukifautia na msemo usemao;’’ ubwabwa mmoja mapishi mengi’’ ,mwanfalsafa huyu iliutoa msemo huu ambao ukiutafasiri katika lugha ya mitindo humaanisha kuwa kito kimoja mitindo tofauti.
Ubunifu na uvaaji katika mitindo ya vito kwa kuzingatia na tamaduni husika umekuwa ukipewa kipaumbele kutokana na kuwa vito hivyo huboresha munekano wa mtu husika,hata hivyo idadi kubwa ya watu imekua ikitilia maanani suala na mitindo ya vito kwa kubuni mitindo ya vito vya asili kama shanga ,bangili n.k pamoja na vito vya kisasa zaidi.
Naendelea kukufuatilia itafika mbali
ReplyDelete